sisi ni nani

ideabank-header

Toka Novemba 1990, Idea Bank Inc. imewaunganisha Wafikiriaji (Wabunifu), Watendaji na Wadhamini katika kuendesha miradi.

Wafikiriaji - ni watu ambao wanajifunza matatizo na kubuni fikra – watafiti, wuanzilishi na wabunifu
Watendaji - ni watu ambao wanashughulika na utendaji – wanamiradi, wanaujenzi na wakurugenzi
Wadhamini - ni watu ambao wanatowa misada – wawekezaji na wasambazaji au watoaji

Sisi ni mtandao ambao unajumuisha Wabunifu, Wanamiradi na Wadhamini katika kuendesha miradi yenye kuwa na lengo la tanzuwa matatizo muhimu. Tunahusika hasa na maswala ya Afya, Mazingira na Mawasiliano.

Tuna kundi la wasaidizi wa miradi wanao andaa watu kikazi, panga mbinu na wanao husika na hela ya kuwezesha kuifanya miradi kuwa kweli. Kundi hili ni la madaktari, mahakimu, wanasayansi, wafikiriaji maarufu, wapasuwaji wa ubongo, wanauchumi na wanamiradi. Ni kweli, Dunia inazidi kukumbwa na majanga mengi na vile vile walimwengu hatuchangayi namna ya tanzuwa matatizo hayo. Kwa hiyo basi, hatuna budi kuhusisha wafikiriaji, watendaji na wadhamini wote pamoja katika swala nzima la kutafuta suluhisho la majanga yanayoikabil dunia.