kazi zetu

ideabank-header2

Idea Bank inatowa huduma muhimu sana: tunaandaa watu kikazi, mbinu za uendeshaji kazi na hela ya kuendesha miradi.

Shughuli (kazi) zetu zimegawanyika katika makundi 4: Vyombo vya tiba; tovuti; anga; viwanja.

Vyombo vya tiba
Fio ndio inahusika na teknolojia ya kutengeneza vyombo vya tiba ambavyo vinaweza kubebwa mkononi. Fio ina makao makuu katika jiji la Toronto, nchini Kanada. Fio inatengeneza vyombo vya tiba vyiwezekanavyo kubebwa kwa mikono, ikiweka pamoja nanoteknolojia, bioteknolojia na teknolojia ya mawasiliano. Vyombo hivyo vina uwezo wa kupima kwa ufanisi mwingi magonjwa ya kuambukia tofauti kwa haraka mno. Hivyo, tukitowa majibu juu majanga mengi yanayo sabanisha vifo vingi sana na kuzidi kuwa pingamizi kuu ya maendeleo duniani. Idea Bank inafanya kazi na Fio ili kuinuwa huduma zake na mitandao yake ya wahenga – wafikiriaji, watendaji, wadhamini – katika vituo vya teknolojia na maeneo ya joto kali yenye kuwa na “pathogen” nyingi.

Tovuti
Huu ni mtandao wa tovuti ambao unawaunganisha wafikiriaji, watendaji na wadhamini ili wujadili matatizo, wachambuwe mawazo yao, watanzuwe matatizo ya aine tofauti na watowe misada. Mradi wa kwanza ni Mtandao wa Mazava, ambao unajishughulisha na magonjwa ya kuambukia. Mradi huu unaendeshwa na Idea Bank ikishirikiana na Fio. Huu mradi upo kwenye tovuti na ni mtandao unao waunganisha wanamirida pamoja na wafikiriaji na wawekezaji.

Anga
Idea Bank inaandaa ndege ambao itakuwa imeundwa na viombo kama vya  zingine ndege za usafiri za kawaida, ndege upanga na ambayo itakuwa nyepesi kuliko chombo chochoto kile cha usafiri wa anga (au mawasiliano ya anga). Lengo muhimu hapa ni la mawasiliano. Madumini yetu ni kutowa huduma za usafiri katika maeneo ambapo hakuna usafiri wa ndege, treni ua meli ama mahali ambapo usafiri ni bei kubwa ama sehemu ambapo kuna ukosefu wa mbinu za usafiri.

Viwanja
Idea Bank inaandaa kuanzisha na kuendesha viwanja ambapo wafikiriaji, watendaji na wadhamini watakuwa wakiweza kukutana, kubadilishana ujuzi na kuzifanyia biashara fikra zao.