historia

madagascar

  • Katika mwezi wa Novemba 1990, Jay Godsall alisafiri Madagascar na huko akakutana na Dr. Nat Quansah ambae alikuwa akishughulika na matatizo ya uchomaji wa pori za Madagascar, na swala uhaba wa fahamu za tiba nchini humo. Huko, Jay alipendekeza wazo (fikra) la kuanzisha Benki Ya Fikra (Idea Bank) ili kuunganisha Waganga wa tiba za Jadi na Madaktari (waganga wa tiba za sasa) katika mtandao mmoja, ambapo fikra zao zingeweza kuchambuliwa na kufanyika “Ujuzi-mali” (fahamu ambazo zimegeuzwa kuwa ujuzi na zenye uwezekano wa kuzwa). Alipo rudi kutoka Madagascar, Jay alianzisha kampuni ambao iliita “Idea Bank.”
  • Mpaka sasa, Idea Bank imeshafanikiwa kuanzisha zaidi ya miradi 25 – hasa katika huduma za Afya, Mazingira na mawasiliano.
  • Katika mwaka wa 2002, Idea Bank imeanza kujishughulisha sana na mahabara (ya nanoteknolojia) na matumizi yake kuhusiana na magonjwa ya kuambukia, mawasiliano na juwa umeme (umeme wa mwionzi ya juwa).
  • Katika mwaka wa 2003, Idea Bank ilikuwa kiungo maalum katika uanzilishaji wa Fio Corporation, kampuni itengenezayo vyombo vitumiwavyo kwenye mahabara wakati wa kupima na kutambua makundi ya magonjwa ya kuambukia.
  • Idea Bank inafanya kazi na Fio pamoja na makundi mengine katika kuchambuwa na kushughulika na miradi ambao inahusiana na manganjwa ya kuambukia, mawasiliano na mwionzi ya juwa.
  • Wakati Idea Bank ikiwa katika utafiti na uchambuzi wa miradi yake, tutawafahamisheni habari chache tu. Tukikamisha kazi zetu, ndipo tutawafahamisheni kwa kiundani. Huku, tovuti yetu na tovuti zingine tunazotumika nazo zitazidi kubaki kimya hadi kazi (miradi) itapokuwa tayari ndo tutaweze kuwapeni habari maalum.